Huduma ya kufunga Mizigo
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro unatoa huduma ya kufungasha mizigo kwa abiria. Huduma hii inatumia plastiki rafiki wa mazingira na inapatikana kulingana na ukubwa wa mzigo husika. Huduma hii inapatikana mara tu baada ya mlango wa kwanza wa ukaguzi wa usalama, upande wa kulia. Kufungasha mizigo husaidia kulinda mizigo yako dhidi ya uharibifu, uchakavu, na michubuko.