Ukaguzi wa Usalama
Abiria wote wanaoondoka, ama Kimataifa au ndani ya nchi, watapitia ukaguzi wa abiria.
Mchakato wa ukaguzi wa abiria
i. Weka vitu vyote vya binafsi, pochi au mikoba katika trei
ii. Weka vitu vya metali (funguo, sarafu) na vya kielektroniki (kompyuta ndogo, simu za mkononi) kwenye trei.
iii. Vua mavazi ya nje yenye uzito mkubwa (km. makoti, jaketi), kofia na vito vya mapambo, na weka kwenye trei.
iv. Weka mizigo yako kwenye mashine ya ukaguzi
v. Wajulishe maafisa wa ukaguzi wa uwanja ikiwa una vifaa vya matibabu, vifaa vya kusaidia au vipandikizi kabla ya kukaguliwa.
vi. Unaweza kuombwa kupitia mchakato wa ukaguzi wa usalama tena hadi maafisa wa usalama watakapojilidhisha.