Huduma ya mizigo iliyopotea
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro unatoa huduma ya kurejesha mizigo ya abiria iliyopotea wakati wa safari. Huduma hii inatolewa na makampuni mawili Swissport na NAS Dar Airco. Ofisi za watoa huduma hawa zinapatikana baada ya eneo la kuchulia mizigo (conveyor belt). Abiria wanakumbushwa kuzingatia kuwa hakuna hakuna malipo yanayotozwa katika huduma hii.