Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

"Inaunganisha Tanzania na Dunia "
TAA Logo

Safiri na Watoto

Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

Safiri na Watoto

Watoto wetu wanapenda kusafiri, hasa furaha ya kutazama ndege zikitia na kupaa. Kama uwanja wa ndege rafiki kwa familia, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro unajitahidi kuhakikisha kwamba watoto wanapata huduma bora ili kujenga kumbukumbu nzuri kuhusu viwanja vyetu vya ndege.

Kusafiri na Watoto Chini ya Umri wa Miaka 2
Watoto walio chini ya umri wa miaka 2 hawahitajiki kuwa na viti vyao wenyewe. Badala yake, wanaweza kupakatwa na wazazi au walezi wakati wote wa safari. Ni muhimu kutambua kwamba abiria mmoja hawezi kuwajibika kwa watoto zaidi ya mmoja. Hakikisha unatoa taarifa kwa shirika la ndege unalopanga kusafiri nalo mapema ili waweze kufanya mipango ya mapema kuhakikisha wanakidhi mahitaji yako ya safari.
Bonyeza hapa kuwasiliana na shirika lako la ndege

Watoto Wanaosafiri Peke Yao
Iwapo mtoto wako anasafiri peke yake, ni muhimu kuwasiliana na shirika la ndege mapema ili kuuliza kuhusu sera na huduma zao kwa watoto wanaosafiri peke yao. Mashirika mengi ya ndege hutoa huduma maalum za kusindikiza na kusimamia watoto wanaosafiri peke yao, kuhakikisha wanatunzwa na kuhudumiwa vyema kutoka wanapofika uwanja wa ndege hadi mwisho wa safari. Hata hivyo, kunaweza kuwa na vikwazo kama vile vikomo vya umri, hivyo ni muhimu kuwasiliana na shirika la ndege kabla ya safari. Hii itakusaidia kuelewa mchakato na mahitaji yoyote au ada za ziada zinazoweza kuhitajika, kuhakikisha safari ya mtoto wako ni salama na inasimamiwa vizuri.
Bonyeza hapa kuwasiliana na shirika lako la ndege