Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, tunatoa kipaumbele na tunaona fahari kuwahudumia abiria wenye ulemavu na changamoto za kimjongeo.
Maegesho Maalum na Vifaa kwa watu wenye elemavu au changamoto za kimjongeo
Tunayo maegesho maalumu yaliyohifadhiwa kwa watu wenye ulemavu, ambayo yapo karibu kabisa na jengo la abiria ili kutoa urahisi wa kupata huduma kwa watu wenye ulemavu. Maegesho haya yameandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa abiria wenye ulemavu wanapata huduma kwa urahisi zaidi.
Kupata Huduma
Ili kufaidika na huduma hizi, abiria wanahitaji kutoa taarifa kuhusu hali yao ya ulemavu wakati wa uhifadhi wa tiketi. Aidha, abiria wanatakiwa kujaza fomu maalum wakati wa uhifadhi ili kusaidia kuelewa mahitaji yao na kuhakikisha maandalizi ya safari yao yanafanyika kwa ufanisi.
Msaada Siku ya Safari
Siku ya kuondoka au kuwasili, wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa KIA watakuwa tayari kukupokea na kutoa msaada wa kina kwa abiria wenye ulemavu. Huduma hizi zitajumuisha msaada wakati wa kujiandaa kuingia kwenye ndege, kusimamia mizigo yao, na mahitaji mengine yoyote yanayoweza kutokea ili kuhakikisha safari inakuwa rahisi na isiyo na msongo.
Ikiwa una changamoto au unahitaji kuwasiliana na shirika la ndege, tafadhali bonyeza hapa.