Duka la Vinyago na Vitu vya Kitamaduni
Katika eneo la wasafiri wanaoondoka kimataifa, kuna maduka ya vinyago na vitu vya kitamaduni. Maduka haya yanakupa fursa ya kununua bidhaa za Kiafrika zilizotengenezwa kwa mikono. Bidhaa hizi zinaweza kutumika kama zawadi kwa wapendwa wako pindi utakaporudi nyumbani. Bidhaa hizi ni kama vile mikufu iliyochongwa kutoka katika mawe, mikufu iliyotengenezwa kutoka katika bidhaa za wanyama kama vile pembe za ng'ombe, pamoja na vitambaa vilivyofumwa kutoka katika malighafi za pamba za Kiafrika na kutengenezwa kwa mikono. Pia, kuna vinyago vilivyochongwa kutoka katika miti migumu kama vile Mpingo. Bidhaa hizi huelezea ubunifu kutoka kwa wachongaji wa Kiafrika.