Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro

"Inaunganisha Tanzania na Dunia "
TAA Logo

Matengenezo ya Ndege

Imewekwa: 28 July, 2024
Matengenezo ya Ndege

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tunajivunia kushirikiana na kampuni ya kuaminika ya matengenezo ya ndege, Direct Maintenance. Kampuni hii imeithinishwa na EASA Part-145, ikijikita katika kutoa huduma bora za matengenezo ya ndege, ikijumuisha uthibitisho wa Release to Service kwa mchanganyiko mbalimbali wa ndege na injini. Ushirikiano wetu na Direct Maintenance unahakikisha ndege zako zinapata huduma bora zaidi, kwa kuzingatia usalama, kutegemewa, na ufanisi.

Uwezo wa Kufanyia Matengenezo ndege za Aina Mbalimbali
Direct Maintenance inatoa huduma kamili za matengenezo kwa ndege mbalimbali kutoka familia za Boeing, Airbus, na Embraer. Hapa chini ni mchanganyiko maalum wa ndege na injini wanazohudumia:

Familia ya Boeing:

  • B737-300/400/500 pamoja na -600/700/800/900 (CFM56)
  • B737-7/8/9 (CFM LEAP-1B) inayojulikana kama “B737 MAX”
  • B747-200/300 (PW JT9/RR RB211/GE CF6-50)
  • B747-400 (PW4000/RR RB211/GE CF6-80)
  • B747-8 (GEnx)
  • B757-200/300 (PW2000/RR RB211)
  • B767-200/300/400 (PW4000/GE CF6-80)
  • B777-200/300 (GE90/RR Trent)
  • B787-8/9 (GEnx/RR Trent)
  • MD11 (PW4000/GE CF6-80)

Familia ya Airbus:

  • A319 (CFM56/V2500/PW1100G)
  • A319 (CFM LEAP-1A) inayojulikana kama “A319NEO”
  • A320 (CFM56/V2500/PW1100G)
  • A320 (CFM LEAP-1A) inayojulikana kama “A320NEO”
  • A321 (CFM56/V2500/PW1100G)
  • A321 (CFM LEAP-1A) inayojulikana kama “A321NEO”
  • A330 (PW4000/RR Trent/GE CF6-80)
  • A340-300 (CFM56)
  • A340-500 (RR Trent)
  • A350
  • A380 (GP7200/RR Trent)

Familia ya Embraer:

  • ERJ-170 series (GE CF34)
  • ERJ-190 series (GE CF34)

Kushirikiana na Direct Maintenance kunatuwezesha kutoa huduma za kipekee za matengenezo ya ndege katika KIA. Timu yao ya wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu inahakikisha kila ndege inapata huduma bora, kuhakikisha shughuli zako zinaendelea kwa ufanisi na bila matatizo

 

Mawasiliano: Ofisi ya KIA
Meneja Matengenezo: Daniel de Dardel, 
Simu: +254 7 2252 5329