Katika kutekeleza dhima yake ya kutoa huduma ya majengo bora kwa Serikali na makazi ya gharama nafuu kwa Watumishi wa Umma kwa kutumia njia bora na fanisi za usimamizi wa Miliki ya Serikali, huduma ya Ushauri na Ujenzi, TBA inaongozwa na misingi ifuatayo;
- Utaalamu: Tunatekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia utaalamu, weledi, maadili na kwa kuzingatia viwango na miongozo ya huduma zetu na kuelewa masuala mtambuka.
- Kujali Mteja: Tunahakikisha tunatoa huduma inayofaa, yenye kuridhisha na kwa muda muafaka kwa wateja wetu.
- Uadilifu: Tunatoa huduma kwa uaminifu wa kiwango cha juu na kuonyesha uthabiti wa kufuata maadili mema katika utekelezaji wa majukumu yetu.
- Kufanya Kazi kwa Ushirikiano: Tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano ili kutimiza malengo yetu.
- Uwazi: Tunatekeleza majukumu yetu kwa uwazi na kwa kuwajibika kwa umma.
- Thamani ya Fedha: Tunahakikisha tunafuata viwango na vipimo stahiki na kwa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu.
- Ubunifu: Tunatumia na kuwezesha matumizi ya teknolojia, mbinu za kisasa na uzoefu ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuimarisha ubora wa huduma zetu.