Kurugenzi hii ina jukumu la usimamizi na uendelezaji wa Miliki yote ya Serikali. Miliki ya Serikali ni pamoja na viwanja/maeneo ya ardhi yaliyotengwa kwa matumizi ya Serikali, Majengo ya ofisi za Taasisi mbalimbali za Serikali, nyumba za viongozi Serikalini na nyumba za kuuza na kupangisha kwa Watumishi wa Umma na Wananchi kwa ujumla. Idara hii inasimamiwa na Mkurugenzi akisaidiwa na Mameneja wa Sehemu tatu ambazo ni Sehemu ya Usimamizi wa Miliki, Sehemu ya Uendelezaji Miliki na Sehemu ya Usimamizi wa nyumba za Umma.
1. Sehemu ya Uendelezaji wa Miliki
Sehemu hii inahusika na kusimamia ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa Umma, majengo ya kibiashara na nyumba za viongozi, kushauri upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya maendelezo ya Miliki na upatikanaji wa nyaraka za kisheria za ardhi, kuwezesha malipo ya kodi ya ardhi, kodi ya majengo na malipo mengine ya ushuru na kushauri masuala ya bima za majengo na ardhi, kusimamia utekelezaji wa ubia na miradi ya uwekezaji na kufanya uthamini wa majengo ya Serikali.
2. Sehemu ya Usimamizi wa Miliki
Sehemu hii inahusika na ukarabati wa nyumba na majengo, kupangisha nyumba za makazi na majengo ya ofisi. Kuwapatia makazi viongozi wa Serikali wenye stahili, kusimamia matumizi bora ya Miliki ya Serikali kwa kuchagua mbadala wa matumizi bora ya Miliki Kuu, kushauri juu ya malalamiko ya wapangaji na kusimamia ustawi wa wapangaji na Kuandaa mpango wa ukusanyaji wa kodi na utaratibu wa kusimamia wapangaji.
3. Sehemu ya Usimamizi wa nyumba za Umma
Kusimamia utekelezaji wa tathmini ya mahitaji ya mpango wa makazi ya Umma, kusimamia ubunifu na utekelezaji wa programu ya makazi ya kutosha kwa watumishi wa Umma, kuainisha maeneo kwa kufanya tathmini zaidi ya utoaji wa makazi ya watumishi wa Umma, kufuatilia na kusimamia ubunifu wa mpango wa makazi ya gharama nafuu na kukuza mpango wa ubunifu na ujenzi wa makazi ya kutosha kwa tabaka na rika zote na kusimamia mchakato wa mauzo ya nyumba za Serikali, kwa kuainisha njia za malipo na kuwezesha uhamisho wa umiliki wa nyumba zilizouzwa.