Kurugenzi hii ina jukumu la kusimamia masuala ya Fedha, Utawala na Rasilimali watu, Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini. Kurugenzi hii inaongozwa na Mkurugenzi akisaidiwa na Mameneja wa Sehemu tatu ambazo ni Sehemu ya Uhasibu na Fedha, Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu na Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini.
1. Sehemu ya Uhasibu na Fedha
Sehemu hii husimamia na kuhakiki malipo kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, miongozo na nyaraka zinginezo na kutunza hesabu na kutekeleza viwango na taratibu mbalimbali za uhasibu.
2. Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
Sehemu hii inahusika na kutunga na kutekeleza sera, taratibu na mikakati ya usimamizi wa rasilimali watu na kuhakikisha kuwa tathmini za utendaji kazi wa watumishi zinafanyika kwa haki na uwazi kulingana na sera na taratibu zilizoidhinishwa.
3. Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini
Sehemu hii inahusika na kuratibu maandalizi ya mpango kazi wa mwaka, mpango wa muda wa kati na mrefu na kuunganisha katika mpango jumuishi wa maendeleo ya Wakala. Kuongoza utayarishaji wa bajeti ya Wakala kwa kuzingatia miongozo na vipaumbele vya kila mwaka wa Serikali na kufanya tathmini ya kiuchumi ya miradi ya maendeleo.