Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Tunafanya Nini

Jukumu kuu la TBA ni kutoa huduma ya makazi kwa Serikali, Watumishi wa Umma na Wananchi kwa ujumla pamoja na huduma za Ushauri na Ujenzi wa majengo ya Serikali. Miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na:

  1. Ujenzi wa majengo mapya ya Serikali.
  2. Matengenezo ya majengo ya Serikali.
  3. Ugawaji au uuzaji  wa nyumba za Serikali kwa watumishi wa Umma.
  4. Kuuza nyumba za Serikali kwa wananchi kwa ujumla kwa miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na sekta binafsi au mkopo kutoka Taasisi za Fedha.
  5. Kupangisha nyumba za Serikali kwa watumishi wa Umma na kibiashara.
  6. Kusimamia  majengo ya Serikali na kuhifadhi kanzidata ya viwanja na majengo ya Serikali.
  7. Kutoa huduma ya Ushauri kwa miradi ya majengo ya Serikali.
  8. Kuidhinisha michoro ya Taasisi za Serikali (MDAs) na kutoa vibali vya ujenzi wa majengo ya Serikali. 
  9. Kuanda na kuweka viwango vya kiufundi na ubora kwa majengo ya Serikali na kufanya mapitio ya mara kwa mara.
  10. Kusimamia majengo yote na mikataba ya Ushauri pamoja na mikataba ya makubaliano ya viwango vya huduma kwa majengo ya Serikali.
  11. Kuhakikisha kwamba kazi zote za ujenzi zinatekelezwa kuakisi thamani ya fedha.
  12. Kutoa huduma za usimamizi wa miradi kwa majengo ya Taasisi za Serikali (MDAs). 
  13. Kutoa huduma ya usimamizi wa matumizi ya majengo kwa Taasisi za Serikali (MDAs).
  14. Kuendesha karakana za Serikali kwa ajili ya kuzalisha samani na bidhaa za mbao na chuma kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya TBA.
  15. Kutoa huduma ya usimamizi wa majengo na udalali.
  16. Kuishauri Serikali kuhusu sera na masuala ya kisheria yanayohusu sekta ndogo ya majengo.