Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Kurugenzi ya Ushauri

Kurugenzi hii inahusika na kutoa huduma za Ushauri kuhusu ubunifu majengo, uhandisi, ukadiriaji majenzi na huduma za majengo. Kurugenzi hii inaongozwa na Mkurugenzi akisaidiwa na mameneja wa sehemu nne ambazo ni Sehemu ya Ubunifu Majengo, Sehemu ya Uhandisi, Sehemu ya Ukadiriaji Majenzi na Sehemu ya Huduma za Majengo.

1. Sehemu ya Ubunifu Majengo

Sehemu hii inahusika na kupitia bunifu za majengo ili kubaini mapungufu ya viwango vya ubinifu na ubora wa vifaa. Kupitia na kuhuisha viwango na miongozo mbalimbali ya ubunifu majengo ya Wakala, kusoma pembuzi yakinifu na bunifu za washauri wengine.


2. Sehemu ya Uhandisi wa Majengo

Sehemu hii inashughulika na kufuatilia miradi ya Wakala ili kubaini mapungufu ya kihandisi na ubunifu wa majengo mbalimbali, kukagua na kuhuisha viwango vya ubora wa majengo ya Wakala na kuthibitisha bunifu za kihandisi zinazoandaliwa na Sehemu hii.

3.Sehemu ya Ukadiriaji Majenzi

Sehemu hii inahusika na kushauri juu ya mapungufu ya viwango vya vifaa vya ujenzi, kupitia, kuhuisha na kushauri juu ya viwango na miongozo mbalimbali ya ukadiriaji majenzi ya Wakala. Kuandaa na kuhuisha mikataba ya matengenezo na miradi ya maendeleo ya Wakala. Kudhibiti na kusimamia miradi ya Wakala, kuthibitisha makadirio ya ujenzi na nyaraka mbalimbali na Kushauri na kushiriki katika uteuzi wa washauri na wakandarasi wanaotoa huduma kwa Wakala.

4. Sehemu ya Huduma za Majengo

 Sehemu hii inahusika na kufanya tathmini ya athari za miradi kwenye mazingira na jamii (ESIA), tathmini ya ubora wa majengo, upembuzi yakinifu wa miradi ya ujenzi na tathmini ya hali ya majengo.