Kurugenzi hii inahusika na ujenzi wa nyumba mpya za Serikali kwa ajili ya watumishi wa umma, Ujenzi wa nyumba mpya kwa ajili ya viongozi wa Serikali, Ujenzi wa majengo ya ofisi kwa Wizara na Taasisi za Serikali, Utengenezaji wa samani kwa ajili ya nyumba za makazi na Ofisi za Serikali na Ukarabati wa nyumba za makazi na majengo ya Ofisi za Serikali. Kurugenzi hii inaongozwa na Mkurugenzi akisaidiwa na Mameneja wa Sehemu mbili ambazo ni Sehemu ya Ujenzi na Sehemu ya Karakana na Matengenezo. Aidha kurugenzi hii imesajiliwa kama Mkandarasi daraja la kwanza na Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB).
1. Sehemu ya Ujenzi
Sehemu hii inahusika na kuanzisha, kuhuisha na kutumia taratibu/miongozo mbalimbali ya ujenzi, kuhakikisha nyaraka za ujenzi zinapitiwa kabla ya ujenzi kuanza/ kujaza nyaraka za zabuni, kuandaa mpangokazi wa utekelezaji wa mradi na kufanya tathmini ya mahitaji ya miradi na kuandaa bajeti.
2. Sehemu ya Karakana na Matengenezo
Sehemu hii inahusika na kufanya tathmini ya mahitaji ya rasilimali, kuandaa bajeti na kukusanya rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa karakana na utekelezaji wa miradi ya matengenezo.