Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

Timu za Shirika la Elimu Kibaha zang`ara.

Imewekwa: 25 Oct, 2024
Timu za Shirika la Elimu Kibaha zang`ara.

Timu za Shirika la Elimu Kibaha zang`ara

Timu ya Soka ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha – Kibaha FDC na timu ya netiboli ya chuo hicho ambazo zinamilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha (KEC) zimepata ushindi mnono katika mechi za kirafiki zilizochezwa viwanja vya Shirika.

Mechi ya soka ilikuwa ni kati ya Kibaha FDC na timu ya Njuweni wakati Timu ya Netiboli ya Kibaha FDC ilikipiga na Timu ya Netiboli ya Njuweni zote kutoka Mkoa wa Pwani.

Timu ya Soka ya Kibaha FDC ilifanikiwa kuichabanga Njweni mabao 4-0 katika mchezo mkali uliovutia, mashabiki wa pande zote mbili ambao walikuwa wakihamasisha ushindi mwanzo mwisho.

Mabao ya wenyeji Kibaha FDC yaliwekwa nyavuni na Babuali Mashaka ambaye alifunga goli la kwanza na la nne, goli la pili Athumani Seif maarufu Ochu na goli la tatu Paschal Lyuba maarufu Duchu.

Wakati timu ya mpira wa miguu ya Kibaha FDC ikitakata katika uwanja wao wa nyumbani, dada zao wawaliwamiminia mvua ya magoli Timu ya Netiboli ya Njuweni bila huruma kwani walitandikwa mabao 40-4.

Timu za Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha, zilipewa zawadi ya jezi pamoja na mpira. Mechi hizo zilifadhiliwa na Vodacom Tanzania.