CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIBAHA
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC)
Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (KFDC) kilianzishwa mwaka 1964 kikijulikana kama `Farmers Training Centre. ` Katika mwaka 1975 wakati vyuo vya maendeleo ya wananchi (Folk Development Colleges) vilipoanzishwa Tanzania nzima, chuo hiki kilibadilishwa jina na kuitwa KFDC chini ya Shirika la Elimu Kibaha. Aidha, hiki ndicho chuo mama na cha mfano kilichowezesha kuanzishwa kwa vyuo vingine vya maendeleo ya wananchi nchini.
Sifa za Kujiunga:
- Kujua kusoma na kuandika
- Mtu yeyote anayehitaji kujiendeleza katika fani yoyote
Kozi za muda mrefu zinazotolewa chuoni:
- Ufundi Umeme
- Ufundi Magari
- Ufundi Uundaji na Uundaji vyuma (Uchomeleaji)
- Ufundi Seremala
- Ufundi Ubunifu na Ushonaji wa Mavazi
- Ufundi Uashi
- Ufundi Bomba
- Kilimo
- Mifugo
- Upishi
Kozi za muda mfupi zinazotolewa chuoni:
- Ufundi Umeme
- Ufundi Magari
- Ufundi Uundaji na Uundaji vyuma (Uchomeleaji)
- Ufundi Seremala
- Ufundi Ubunifu na Ushonaji wa Mavazi
- Ufundi Uashi
- Ufundi Bomba
- Kilimo
- Mifugo
- Upishi
- Matumizi ya kompyuta
- Ujasiriamali
- Aluminium
- Udereva
Chuo kina mazingira mazuri, kipo eneo linalofikika kwa urahisi, huduma za maji na umeme ni za uhakika.
Chuo kina nafasi za kutwa na za bweni kulingana na mahitaji ya mwanachuo.
Muhula wa masomo huanza Januari kila mwaka na fomu zinatolewa chuoni kuanzia mwezi Oktoba. Kozi fupi hutolewa muda wote.