BODI YA WAKURUGENZI
Bodi ya Wakurugenzi
Ibara ya 6 ya kuanzishwa kwa Shirika La Elimu Kibaha, GN Na. 2 ya mwaka 1970, iliyototolewa chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma, Sura 257, R.E. 2002, inatoa utaratibu wa usimamizi wa Kituo kupewa Bodi ya Wakurugenzi. Bodi inajumuisha wawakilishi kutoka Wizara zinazohusika kwa wakati huo ambazo ni Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu ya Taifa, Wizara ya Fedha na Utawala wa Mikoa; na Kamishna wa Wilaya (Kibaha) ambapo Kituo kilipo na wanachama wengine watatu walioteuliwa na Bodi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkurugenzi ndiye Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi na anawajibika kwa Bodi ya Wakurugenzi. Yeye anateuliwa na Waziri mwenye dhamana na Utawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa.