Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

MENEJIMENTI

Menejimenti

Kamati ya Uongozi

Menejimenti inasimamia majukumu mbalimbali ya Shirika la Elimu Kibaha na inajumuisha wajumbe 12; Mkurugenzi Mkuu, Wakurugenzi 5, na Wakuu wa Vitengo 7 ambao wote wanawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu. Kurugenzi zinazohusika kuunda Menejimenti ni Kurugenzi ya Huduma za Elimu, Kurugenzi ya Maendeleo ya Jamii, Mafunzo na Uzalishaji, Kurugenzi ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, na Kurugenzi ya Fedha na Uhasibu. Vitengo vinavyounda Menejimenti ni Kitengo cha Huduma za Kisheria, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Kitengo cha Uhusiano, Mawasiliano na Masoko, Kitengo cha Miliki na Majengo, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi na Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.