MAKTABA YA UMMA KIBAHA
Maktaba ya Umma Kibaha
Maktaba ya Umma Kibaha ilianzishwa mnamo Julai 1965. Maktaba hii ipo chini ya usimamizi wa Kurugenzi ya Huduma za Elimu. Bonyeza hapa kwa muundo kamili. Pia, inatambulika kama Maktaba ya Mkoa wa Pwani.
Majukumu ya maktaba hii ni kutoa taarifa na huduma za marejeleo kwa watumiaji wa umma yakiwemo; upangaji, ununuzi, kuwezesha, kuandaa, kutoa, kuhifadhi na kushauri masuala yote yanayohusiana na rasilimali na huduma za maktaba.
Maktaba ina takriban machapisho 25,250 vikiwemo vitabu vya marejeleo, majarida na miongozo, picha za matukio, CD, DVD na kanzidata mbalimbali za kitaifa na kimataifa kutoka katika mitandao kama vile; springerlink, Bioline International, Elsevier, EconBiz, Researchgate na mitandao mingine mbalimbali.
Maktaba ipo wazi kwa watumiaji wa ndani na nje, siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 3.00 asubuhi - 12.00 jioni na Jumamosi kuanzia 3:00 asubuhi – 9:00 alasiri isipokuwa siku za Jumapili na Sikukuu.
Maktaba hii ina jukumu muhimu katika kutoa huduma mbalimbali kwa watumiaji ili kukidhi mahitaji yao. Pia, inasaidia kazi ya utafiti kwa watumiaji, huku wanafunzi kutoka shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu wakitumia maktaba kwa madhumuni ya marejeleo mbalimbali.