Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

KITUO CHA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO TUMBI

Kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto Tumbi

Kituo kilianzishwa mwaka 1969 kwa namba za usajili 0102, kikiwa chini ya Kurugenzi ya Huduma za Elimu.

Malengo ya kuanzishwa kwa kituo: 

  1. Kusimamia makuzi na malezi ya watoto
  2. Kuwapatia elimu bora ya awali
  3. Kuwajengea uwezo wa kujitegemea
  4. Kuwapatia lishe na afya bora

Kituo ni cha kutwa, mchanganyiko wasichana na wavulana, kina uwezo wa kupokea watoto mia moja na ishirini (120)

Huduma zinazotolewa ni:

  1. Elimu ya dini
  2. Utamaduni
  3. Zana za kihisabati
  4. Kutunza afya na mazingira
  5. Kuwasiliana
  6. Stadi za sanaa na michezo 

Namna ya kujiunga na kituo

Tunatoa fomu za kujiunga kuanzia mwezi (Novemba) kila mwaka.