Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

SHULE YA SEKONDARI TUMBI

Shule ya Sekondari Tumbi

Shule ya Sekondari Tumbi ni Shule ya Serikali ya Umma inayomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha na ipo chini ya Kurugenzi ya Huduma za Elimu. Shule hii ilianzishwa Januari mwaka 2007 na kupatiwa namba ya usajili S.940, ni mchanganyiko wasichana na wavulana.

Shule hii ipo Mtaa wa mkoani A, Kata ya Tumbi katika Halmashauri ya Wilaya ya mji Kibaha. Shule ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 950 na inatoa elimu ya kidato cha kwanza mpaka cha nne.

Huduma zinazotolewa

Shule inafundisha masomo ya sayansi ambayo ni; Chemia, Biolojia, Fizikia, Hisabati, na Maarifa ya nyumbani. Pia, shule inafundisha masomo ya sanaa ambayo ni kingereza, Kiswahili, Historia, Jiografia, Uraia na masomo ya biashara.

Mafanikio

Shule ina mafanikio makubwa kitaaluma ambayo yametokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la ufaulu.

Kujiunga na shule

Wanafunzi wanaojiunga na Shule ya Sekondari ya Tumbi, wanachaguliwa na Serikali.