Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA

Shule ya Sekondari Kibaha

Shule ya Sekondari Kibaha ni Shule ya Serikali ya Umma ambayo inamilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha na kusimamiwa na Kurugenzi ya Huduma za Elimu. Shule hii ilianzishwa mwaka 1965, wakati shule ikianzishwa, ilikuwa na wanafunzi 110 wa kidato cha kwanza na wanafunzi 60 wa kidato cha tano. Shule ipo Mkoa wa Pwani, Halmashauri ya Kibaha Mji, Kata ya Tumbi Mtaa wa Mwanalugali A. Shule hii ni ya wavulana na wanafunzi wote ni wa bweni. Shule ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 840.

Huduma zinazotolewa

Shule ya Sekondari Kibaha inafundisha wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha sita na kutoa malezi bora ambayo yanawawezesha wanafunzi wetu kuwa na tija katika jamii baada ya kuhitimu. Pia, tunaendesha mafunzo ya kitaaluma na tunafundisha shule zilizopo nje ya Mkoa wa Pwani, Tanzania Bara na Visiwani kwa kutumia madarasa janja (smart class).

Masomo yanayofundishwa ni pamoja na Uraia, Historia, Jiografia, Kiswahili, Kiingereza, Biolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Kilimo na Masomo ya Biashara. Kwa upande wa kidato cha tano na sita tuna michepuo ifuatayo; PCM, PCB, PMCs, CBA na ECA.

Mafankikio

Shule hii, imefanikiwa kutoa wahitimu ambao wameshika nafasi mbalimbali za uongozi kitaifa na kimataifa. Mfano, ni aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine.

Tunazalisha wahitimu wenye nidhamu, wazalendo na waadilifu ambao wanakubalika katika jamii.

Tunajishughulisha na upandaji miti maeneo yote ya shule kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kuboresha afya za wanafunzi na jumuiya yote kwa kupanda miti ya matunda na kulima bustani za mbogamboga.

Tunashiriki mashindano kupitia klabu mbalimbali kwa mfano; TRA, STEM, UN, TAXI, FEMA, HEATH AND ENVIRONMENT, UWEZO na ICLD na kupata tuzo mbalimbali.

Namna ya kujiunga na shule

Shule ya Sekondari Kibaha ni shule maalumu na wanafunzi wanapangwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kulingana na sifa husika.