MAJUKUMU YA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA
Majukumu ya Shirika la Elimu Kibaha
Malengo ya kuanzishwa kwa Shirika la Elimu Kibaha ni kutoa huduma za afya, huduma za elimu na huduma za stadi za kilimo kwa njia ya Kushabihiana na Kushabikiana. Majukumu ya kuanzishwa Shirika, yameainishwa katika aya ya nne (4) ya Tangazo la Serikali Na. 02/1970 kama ifuatavyo:
1. Kwa idhini ya Bodi ya Nordic, kuchukua dhamana na madeni ya mradi na kutekeleza shughuli zote za mradi
2. Kukuza maendeleo ya kilimo ikiwa ni pamoja na kutoa taaluma na mafunzo ya kilimo kwa vitendo na uzalishaji wa chakula
3. Kufundisha na kutoa vifaa tiba kwa wanafunzi wa tiba, wauguzi na wahudumu wa afya wa vijijini ili kuzuia magonjwa
4. Kutoa elimu kwa jamii juu ya afya ya jamii na usafi wa mazingira
5. Kutoa huduma au usaidizi wa afya katika maeneo mengine ya nchi ambako Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii au kitivo cha dawa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa pamoja wataona ni lazima kuanzishwa kwa kuzingatia madhumuni ya uanzishwaji wa Shirika la Elimu Kibaha
6. Kutoa Elimu ya Sekondari kwa mujibu wa sera, sheria na kanuni zinazosimamia elimu
7. Kuingia kwenye makubaliano ya kufanya kazi ambazo Bodi imeona zitasaidia kuboresha utendaji, uendeshaji na kuleta ufanisi katika Shirika