Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA KIBAHA

Shule ya Wasichana Kibaha

Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha (Kibaha Girls Secondary School), ni shule ya umma na ipo chini ya Kurugenzi ya Huduma za Elimu, Shirika la Elimu Kibaha (KEC). Shule hii ilianzishwa kwa ajili ya wasichana na ilisajiliwa mwaka 2007 kwa namba S.3880.

Huduma zinazotolewa

Elimu ya sekondari inatolewa kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne kwa mchepuo wa masomo ya Sanaa, Sayansi na Biashara.

  Mafanikio:

  • Shule imefanikiwa kuwaendeleza wanafunzi kitaaluma na wamefanikiwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo mbalimbali nchini.
  • Shule ilishiriki katika mashindano ya ‘Tax club quiz competition’ kwa mfano mwaka 2023 shule ilikuwa mshindi wa tatu kitaifa.
  • Shule ilishiriki katika mashindano ya miradi “projects” za “young scientists Tanzania” kwa mfano mwaka 2022 iliibuka na kuwa mshindi wa kwanza kitaifa.

Kujiunga na shule

Wanafunzi wanaojiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Kibaha, wanachaguliwa na Serikali.