KCOHAS yapongezwa.

Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Kamal Group, Bw. Satyam Gupta amelipongeza Shirika la Elimu Kibaha kupitia Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha (KCOHAS) kwa kuwawezesha wanachuo kufanya vizuri mfululizo katika mitihani yao ya Taifa.
Hayo yamesemwa na Bw. Gupta wakati wa mahafali ya 57 ya KCOHAS yaliyofanyika kwenye Viwanja vya chuo hicho.
Bw. Gupta ameahidi kutatua changamoto zilizopo katika chuo hicho kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Katika risala iliyosomwa na mmoja wa wahitimu hao, amesema wanachuo wamepata mafanikio kwa njia ya kujifunza kwa nadharia na vitendo pamoja na kutoa msaada kwa watoto yatima wanaoishi kuzunguka Shirika la Elimu Kibaha.
Wanachuo hao pia wamepongeza uongozi wa Shirika kwa kujenga madarasa yenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 70 kwa wakati mmoja kwa kutumia mapato ya ndani.
Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha, Bw. Lusungu Nyagawa amemshukuru mgeni rasmi kwa kukubali kufika katika mahafali hayo.