Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

Shirika La Elimu Kibaha

SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LAWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA

Imewekwa: 30 Apr, 2025
SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA LAWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC), Bw. Anneth Nnko amewapongeza watumishi 13 wa vitengo pamoja na kurugenzi kwa kuchaguliwa kuwa watumishi hodari wa mwaka 2024/2025 wakati wa sherehe za Mei Mosi zilizoazimishwa kimkoa kwenye Uwanja wa Shirika.

 Aidha katika sherehe hizo Bw. Novathi Mizungwe amechaguliwa kuwa mtumishi bora wa jumla kwa mwaka 2024/2025 kwa Shirika la Elimu Kibaha.

 Katika sherehe hizo, Bw. Nnko amewataka watumishi wa Shirika waendelee kudumisha ushirikiano ili waweze kufanya kazi kuwa bora.