Naibu Waziri TAMISEMI alipongeza Shirika la Elimu Kibaha

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi, Zainab Katimba (Elimu) ameipongeza timu ya menejimenti ya Shirika la Elimu Kibaha kwa kusimamia utoaji wa huduma bora ya elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari, wanachuo wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha na Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC).
“Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha kina mchango mkubwa katika nchi hii kwa sababu kinatoa wataalamu bora wa afya ya msingi ambao wanawahudumia asilimia 75 ya Watanzania wanaohitaji huduma za afya,” amesema Bi. Zainab Katimba.
Akizungumzia Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kibaha (Kibaha-FDC), Bi. Katimba amesema kuwa tayaria Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeaanza kukarabati chuo hicho ili kiwe na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia ili kiweze kudahili wanafunzi wengi zaidi.
Pia, Naibu Waziri amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha, Bw. Robert Shilingi kwa kutumia mapato ya ndani kutekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha pamoja.