Maktaba ya Umma Kibaha
Maktaba ya Umma Kibaha
Shirika hutoa huduma mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na watu wazima. Huduma zinazotolewa ni:
- Nafasi ya kusoma
- Usajili wa watumiaji wapya
- Mafunzo kwa watumiaji
- Huduma za uazimishaji vitabu na maandiko mbalimbali
- Huduma ya uazimishaji kati ya maktaba na maktaba
- Huduma za ushauri wa namna ya uendeshaji wa maktaba na uandaaji wa machapisho katika shule
- Huduma za watoto
- Huduma za mtandao
Watumiaji Wetu
Jamii yote ya Shirika la Elimu Kibaha na jumuiya inayozunguka wana haki ya kutumia maktaba.
Ada ya uanachama kwa mwaka kwa watumiaji wa nje ni:
i. Mtu mzima
Wananchi Tshs. 10,000/= Mgeni US $ 25
ii. Wanafunzi wa shule ya sekondari
Wananchi Tshs. 7,000/= Mgeni US $20
iii. Wanafunzi wa shule ya msingi
Wananchi Tshs. 5,000/= Mgeni US $20
Ada ya uanachama kwa siku kwa watumiaji wa nje
i. Mtu mzima
Wananchi Tshs. 1,000/= Mgeni US $ 2
ii. Wanafunzi wa shule ya sekondari na wanafunzi wa shule ya msingi
Wananchi Tshs. 500/= Mgeni US $ 1