Karibu
Karibu Shirika la Elimu Kibaha
Shirika la Elimu Kibaha, tumejizatiti katika kukuza ubora wa kitaaluma, kuhamasisha ubunifu, na kukuza jamii yenye nguvu. Pia, Shirika linaiwezesha jamii na mtu mmoja mmoja kustawi kimaadili na kitaaluma.
Tovuti yetu imeanzishwa ili kuwezesha jamii kupata taarifa sahihi na kujua huduma mbalimbali zinazopatikana Shirika. Katika tovuti hii utapata maelezo ya udahili wa wanafunzi na kozi zinazotolewa kwenye vyuo vyetu na masomo yanayofundishwa kwenye shule zetu.
Tunaamini katika utoaji wa elimu bora yenye ubunifu, mafunzo, huduma za afya, na mazingira rafiki ya uwekezaji kupitia matumizi bora na yenye ufanisi wa rasilimali zilizopo kwa maendeleo endelevu. Shirika la Elimu Kibaha, linaunga mkono jamii kwa kuwajenga wanafunzi wanaotafuta maarifa, ubunifu, na uvumbuzi wa leo na siku zijazo.
Tunakukaribisha kutembelea tovuti yetu ili utambue uwezo wa Shirika la Elimu Kibaha katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na wadau mbalimbali.
Asante kwa kutembelea tovuti yetu.
Karibu,
Shirika la Elimu Kibaha.